Skip to main content
Skip to main content

Ruto ataka masomo ya Madrasa yatambuliwe rasmi

  • | Citizen TV
    208 views
    Rais William Ruto ameielekeza Wizara ya Elimu kuandaa mfumo wa kuunganisha masomo ya Madrasa na Mpango wa Mafunzo kwa Jamii za Wafugaji katika mfumo rasmi wa elimu nchini. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wanafunzi wa Kaskazini mwa Kenya na maeneo mengine yaliyotengwa wanapata elimu inayotambuliwa rasmi na kufungua fursa zaidi za masomo na ajira. Akizungumza mjini Wajir, Rais alisema mifumo mbadala ya elimu imekuwa ikikosa utambuzi rasmi kwa miaka mingi, hali iliyowanyima maelfu ya wanafunzi nafasi ya kuendelea na masomo yao. Rais alisisitiza kuwa serikali imejitolea kuondoa vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa elimu jumuishi kwa jamii zote nchini.