Rais William Ruto amewaonya wasimamizi wa shule dhidi ya kuwatuma wanafunzi nyumbani kutokana na changamoto za ulipaji karo, akisisitiza kwamba serikali imesambaza shilingi bilioni 44 ili kufadhili elimu ya umma. Rais Ruto aliwahakikishia wanafunzi na wazazi kwamba serikali yake imewajibika kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu nchini. Aidha Rais Ruto alitoa wito kwa wakazi kuthamini siasa za maendeleo zisizo na ukabila na migawanyiko, akisema amejitolea kutekeleza ajenda alizoafikiana na marehemu Raila Odinga.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive