Rwanda yakubali kuwahifadhi wahamiaji 250 kutoka Marekani

  • | BBC Swahili
    1,080 views
    Marekani na Rwanda zimekubaliana kuwa nchi hiyo ya Afrika itapokea hadi wahamiaji 250 waliofukuzwa kutoka Marekani, msemaji wa serikali ya Rwanda na afisa mmoja aliliambia shirika la Reuters, huku utawala wa Rais Donald Trump ukichukua mkondo mkali juu ya wahamiaji. Ikulu ya White House na Wizara ya Mambo ya Nje haikutoa maoni mara moja huku Idara ya Usalama wa Taifa ikielekeza maswali yaulizwe kwa Wizara ya Mambo ya Nje. Awali Rwanda ilikuwa na ushirikiano wa kuwapokea wahamiaji kutoka Uingereza uliosimamishwa na mahakama kuu ya Uingereza hata baada ya serikali ya nchi hiyo kuilipa Rwanda mamilioni ya pauni kuendeleza mpango huo. Swali ni je, mpango huu utatekelezwa vipi? Na una tofauti gani na ule wa Uingereza? Rwanda na Marekani wanafaidika vipi? @RoncliffeOdit anaangazia hili na mengine Mengi leo saa tatu usiku katika Dira ya Dunia TV, itakayokujia mubashara kupitia ukurasa wa YouTube BBC Swahili. #bbcswahili #marekani #rwanda Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw