17,938 views
Duration: 3:10
William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga wamefanya mikutano na wawakilishi wadi wa kaunti ya nairobi kujaribu kutafuta muafaka kati ya Gavana Johnson Sakaja na wawakilishi wadi. Kwenye mkutano huo, sakaja ameahidi kuwashirikisha wawakilishi wadi kwenye mipango yote. Wawakilishi wadi walikuwa wanapania kuwasilisha mswada wa kumtimua sakaja kwa madai kuwatenga kwenye miradi ya maendeleo. Na kama anavyoarifu stephen letoo, ruto na raila wamempa sakaja siku sitini kutatua mzozo kuliopo.