- 1,775 viewsDuration: 1:53Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja anaongoza mpango wa kubomoa ukuta wa Ikulu ya Nairobi ulioko kwenye ardhi ya mkondo wa mto, katika jitihada za kurejesha Mto Nairobi. Kulingana na sakaja, Sehemu ya ukuta wa Ikulu iliyojengwa kwenye ukingo wa Mto Kirichwa pamoja na majengo yote yaliyoko kwenye mkondo wa mto nairobi yatabomnolewa. Gavana Sakaja pia ameeleza kuwa hatua hiyo ni ishara thabiti ya uongozi, akibainisha kuwa Rais, amekubali kufuata kanuni za mazingira.