- 170 viewsDuration: 1:59Serikali imetakiwa kuwapa watu wanaoishi na ulemavu nafasi ya kutumia bahari na raslimali zake katika Kaunti ya Kilifi ili waweze kufaidika na sekta ya uchumi samawati. Wakizungumza katika Hafla ya kuwapa nafasi watu wanaoishi na ulemavu kufika katika ufuo wa bahari na kujihusisha na michezo tofauti tofauti, wadau wamesema ni wajibu wa serikali kumpa nafasi kila mkenya katika kuchangia sekta zote za uchumi licha ya hali Yao. Hafla hiyo iliandaliwa katika ufukwe wa Vidazini mjini Kilifi.