- 366 viewsDuration: 1:34Serikali inapania kuongeza hekari za miwa katika kaunti ya Tana River kutoka 75 hadi 450 baada ya jaribio la kilimo hicho eneo hilo kuonyesha matumaini. Waziri wa maji Erick Mugaa ambaye alizuru shamba hilo amesema serikali itashirikiana na wawekezaji kuzalisha sukari kwenye hekari 50,000 chini ya mradi wa unyunyizaji maji na kupunguza uhaba bidhaa hiyo nchini. Aidha kilimo hicho kinatarajiwa kuongeza nafasi ajira kwa wenyeji.