Serikali kuhitajika zaidi ya shilingi bilioni thelathini kwa ajili ya masomo kwa wanafunzi

  • | KTN News
    320 views

    Serikali itahitaji zaidi ya shilingi bilioni thelathini kwa ajili ya masomo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu, vyuo vya ualimu na vile anuwai na ufundi. Kulingana na ripoti ya matokeo ya mchujo wa kuwateua na kuwatuma wanafunzi walioufanya mtihani wa KCSE mwaka jana katika vyuo vya elimu ya juu, jumla ya wanafunzi laki mbili na elfu hamsini wameteuliwa kujiunga na vyuo tofauti, kwa gharama ya serikali. Hata hivyo ripoti hiyo haijafafanua waliko wanafunzi wengine zaidi ya nusu milioni.