- 179 viewsDuration: 2:42Serikali ya Kaunti ya Laikipia imeahidi kutoa msaada wa haraka kwa wafanyabiashara walioathiriwa na moto wa hivi majuzi katika Soko Jipya la Nanyuki. Akizungumza mjini Nanyuki, gavana wa Laikipia Joshua Irungu alitoa ahadi hizo baada ya kukutana na wafanyabiashara walioathirika ili kutathmini kiwango cha hasara na kujadili mipango ya kuwasaidia.