- 2,072 viewsDuration: 3:02Mahakama ya Kisumu imeiamrisha serikali kulipa fidia ya shilingi milioni thelathini na nane kwa waathiriwa ishirini na wanane wa maandamano ya mwaka 2023. Jaji Alfred Mabeya amesema baadhi ya washtakiwa, ikiwemo idara ya polisi NPS walikiuka vipengee muhimu vya katiba na kusababisha vifo na majeraha kwa waathiriwa. Kwenye uamuzi huo, idara ya polisi imetakiwa kubuni kanuni za kuhakikisha kuna usalama wakati wa maandamano ili kuzuia maafa.