Skip to main content
Skip to main content

Serikali yaimarisha ulinzi dhidi ya Ebola nchini

  • | Citizen TV
    247 views
    Waziri wa Afya Aden Duale amesema kuwa licha ya Kenya kutorekodi kisa chochote cha ugonjwa wa Ebola, serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wananchi wanakingwa dhidi ya maambukizi hayo. Kulingana na Duale, mamia ya watu waliobainika kuwa na dalili zinazofanana na Ebola wamefanyiwa vipimo, huku maelfu ya wasafiri wakikaguliwa katika mipaka mbalimbali nchini kama sehemu ya hatua za tahadhari. Wakati huo huo, viongozi kutoka eneo la Nyanza wameitaka serikali kuimarisha ufuatiliaji na hatua za kinga katika ukanda wa Ziwa Victoria kutokana na shughuli nyingi za usafiri na biashara zinazofanyika katika eneo hilo.