- 338 viewsDuration: 1:32Serikali imetangaza mipango ya kuajiri walimu 16,000 mwezi Julai ili kuziba pengo la uhaba wa walimu nchini. Akizungumza wakati wa hafla ya elimu katika Shule ya Sekondari ya Agenga katika Kaunti ndogo ya Nyatike, Mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Kosgei, alielezea wasiwasi wake kuhusu uhaba huo, na kusema kuwa hali hiyo inaweza kudidimiza viwango vya elimu iwapo haitashughulikiwa.