Skip to main content
Skip to main content

Serikali yatangaza miradi mipya ya maendeleo Wajir

  • | Citizen TV
    385 views
    Serikali imetangaza kuanzishwa kwa miradi kadhaa ya maendeleo katika eneo la Kaskazini Mashariki, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege na chuo kikuu katika Kaunti ya Wajir. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kubadilisha sura ya eneo hilo ambalo limeachwa nyuma kimaendeleo kwa miaka mingi. Akizungumza katika sherehe za Madaraka Dei mjini Wajir, Rais William Ruto alisema miradi hiyo itachochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha huduma kwa wananchi. Rais pia alitangaza kuundwa kwa Kampuni ya Kitaifa ya Mifugo, ambayo itasaidia upatikanaji wa malisho na kuboresha masoko ya mifugo ili kuongeza mapato ya wafugaji nchini.