- 1,231 viewsDuration: 3:20Huku soko la kimataifa la mafuta likiyumba kutokana na misukosuko iliyosababishwa na mzozo wa Mashariki ya Kati, waziri wa kawi Opiyo Wandayi amejitokeza kutetea hatua zilizochukuliwa na serikali ya Kenya. Wandayi anasisitiza kuwa bila mipango ya serikali ya kupunguza ushuru na mfumo wa G-to-G wa ununuzi wa mafuta, bei ya bidhaa hiyo muhimu ingefikia kiwango cha kuwa mzigo ambao wananchi hawangeweza kumudu.