SERIKALI YAWEZA KUONGEZA USHURU KUFANIKISHA MALENGO YA MAPATO

  • | K24 Video
    51 views

    Serikali huenda ikaongeza ushuru ili kufanikisha shughuli zake, kufuatia ripoti iliyowasilishwa kwa Kamati ya Fedha ya Bunge. Katibu wa Hazina, Chris Kiptoo, amesema kuwa serikali mara nyingi haijafikia malengo ya ukusanyaji wa kodi. Serikali inatarajia kukusanya KSh trilioni 3.3 licha ya kukosa kufikia kiwango kilichotarajiwa mwaka huu wa kifedha.