Shamba la ekari 10 laharibiwa Gwetembe Transmara Kusini

  • | Citizen TV
    511 views

    Hali imeendelea kuwa tete katika mpaka wa Transmara Kusini na eneo la Gwetembe Kuria Mashariki baada ya watu wasiojulikana kuharibu shamba la mahindi la zaidi ya ekari kumi eneo hilo. Uharibifu huu ukiripotiwa kufuatia uhasama kati ya jamii zinazoishi eneo hili la mpakani. Na kama Chrispine Otieno anavyoarifu, wakaazi sasa wanamtaka waziri wa usalama Kithure Kindiki kuingilia kati kabla ya hali kuwa mbaya