- 179 viewsDuration: 1:57Baadhi ya wakazi wa milima elgon wameitaka serikali na mashirika ya kijamii kuendeleza vita dhidi ya dhulma za kijinsia baada mpango uliokuwa ukifadhiliwa na shirika la msalaba mwekundu kufikia tamati. Wakizungumza kwenye hafla ya sherehe za kufunga mpango huo kule Cheptais Mlima Elgon,wakazi hao walilipongeza shirika la msalaba mwekundu kaunti ya Bungoma na kusema juhudi zaidi zinahitajika ili kutokomeza dhulma za kijinsia eneo hilo.