- 116 viewsDuration: 1:39Makocha zaidi ya thelathini kutoka kaunti ya Garissa wameanza kupokea mafunzo ya siku tano kupitia shirikisho la kandanda nchini FKF kuhusu kanuni na sheria za kuendesha mchezo wa soka katika kaunti hiyo. Lengo kuu la mafunzo hayo ni kurejesha nidhamu kwenye mchezo huo kando na kuboresha viwango vyake mbali na kutambua vipaji vya wachezaji wa kaunti hiyo. Kupitia kwa mafunzo hayo, timu zote za kaunti hiyo zitatakiwa kuonyesha mchezo wa hali ya juu na kufikia viwango vya kitaifa kwenye michuano ya ligi zao mashinani.