Skip to main content
Skip to main content

Shughuli ya kufukua kaburi linalodaiwa kuwa na maiti Kericho 14 imeanza

  • | Citizen TV
    4,836 views
    Duration: 1:11
    Shughuli za kufukua maiti 14 iliyozikwa katika eneo la makaburini mjini Kericho imeanza rasmi ikiongozwa na mkuu wa DCI, kitengo cha kesi za mauaji Martin Nyuguto. Hii ni baada ya mahakama kutoa idhini ya kufukuliwa kwa kaburi hilo. Inadaiwa kuwa maiti zaidi ya arobaini ilizikwa katika kaburi la pamoja mnamo tarehe 20 mwezi Machi mwaka huu katika eneo hilo la Makaburini. Siku ya Jumatatu mahakama iliamuru watu wawili waliohusishwa na kaburi hilo la halaiki kuzuiliwa kwa siku thelathini ili kuwapa polisi muda wa kutosha kukamilisha uchunguzi wao.