Skip to main content
Skip to main content

Shule kadhaa hazina vitabu vya Gredi 10, baadhi ya wanafunzi wakitumia kwa vikundi

  • | Citizen TV
    301 views
    Duration: 3:03
    Wanafunzi wa gredi ya kumi wamekamilisha muhula wa kwanza huku suala la ukosefu wa vitabu vya kutosha likisalia kuzua wasiwasi. Wazazi wanahofia kuwa watalazimika kuingilia kati na kununua vitabu ili kuhakikisha masomo ya wana wao hayaathiriki. Kwa mujibu wa idara ya mtaala - kicd, hali hiyo inasababishwa na ukosefu wa data sahihi ya wanafunzi walioripoti katika shule zilizoathirika. Na kama anavyoarifu emily chebet, wakuu wa shule hizo wametakiwa kutuma data ya wanafunzi wao na idadi ya vitabu ambavyo havijawafikia.