Siha na maumbile | Ugonjwa wa saratani ya matiti nchini

  • | Citizen TV
    260 views

    Idadi kubwa ya wanawake wanaoishi nje ya miji wameoneka kwenda hospitalini kutafuta matibabu ya saratani ya matiti wakati ambapo saratani hiyo imeenea sana. Hii ni kutokana na ukosefu wa hamasisho ya kutosha kuhusiana na ugonjwa huo ambao umeonekna kuchangia idadi kubwa ya vifo vya kina mama haswa wenye umri wa makamo. Katika siha na maumbile wiki hii mwanahamisi hamadi anatujuza mengi kuhusiana na saratani hiyo baada ya kuzuru kituo cha matibabu cha equity afia tawi la upperhill.