- 44,566 viewsDuration: 8:25Mwaka mmoja baada ya maandamano na ghasia kubwa zilizofuatia uchaguzi wa Oktoba 2025 nchini Tanzania, familia zinaendelea kuomboleza wapendwa wao waliouawa katika machafuko hayo, huku manusura wengine wakiishi na majeraha yaliyobadilisha maisha yao ikiwa ni pamoja na kushindwa kujigharamia matibabu. Ripoti mpya ya Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International imeishutumu serikali kwa kushindwa kuwawajibisha waliohusika na vifo vya waandamanaji jambo ambalo serikali ya Tanzania imekua ikikanusha. Mamlaka nchini Tanzania hazikujibu ombi la BBC la kuhusu madai hayo. Mwandishi wetu Alfred Lasteck amezungumza na familia ambazo bado zinatafuta haki na majibu kuhusu wapendwa wao waliopotea Chapters 00:00 - 00:30 Mwaka mmoja baada ya matukio ya Uchaguzi 00:30 - 01:15 Familia zinatafuta majibu 01:15 - 02:20 Mama amlilia binti yake 02:20 - 2:44 Mwaka mmoja baadaye 02:44 - 3:43 Muathiriwa aliyenusurika kuuawa 03:44 - 04:50 Familia ilivyompoteza baba wa familia 04:51 - 5:45 Familia inahoji mwili wa ndugu yao upo wapo? 5:56 - 6:15 kukarabatiwa kwa miundombinu iliyoharibiwa 06:16 - 07:09 Serikali ikubali makosa? 07:10 - 07:30 Nani anawajibika na vifo? 07: 57 - 08:24 Familia zinasema bado zinamaumivu #bbcswahili #oktoba29 #tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw