Skip to main content
Skip to main content

Tazama mwanaume anayelala na kunguni

  • | BBC Swahili
    58,466 views
    Duration: 1:23
    Mwanasayansi mmoja amekuwa akilala na kunguni kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, akisema kuwa kung'atwa na wadudu hao "hakumsumbui hata kidogo". Mtaalamu wa wadudu, Dkt Richard Naylor, anafuga maelfu ya kunguni kwa ajili ya kufanyia majaribio bidhaa mbalimbali za kudhibiti wadudu kutoka sehemu tofauti za dunia, huku yeye mwenyewe akijitolea kuwa mtu wa kufanyiwa majaribio hayo. Naylor, ambaye ameanzisha jengo maalumu lenye vyumba viwili vya kulala katika bustani ya nyumba yake, eneo la Forest of Dean, Gloucestershire nchini Uingereza, anaeleza kuwa hulazimika kulala pamoja na kunguni hao ili kubaini kama dawa mpya za kunyunyizia na bidhaa za kuwafukuza wadudu hao zinafanya kazi kwa ufanisi Mwandishi wa BBC @ahmedbahajj na taarifa hii Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw