Tume ya EACC yawakamata washukiwa saba kuhusiana na madai ya ufisadi katika kaunti ya Isiolo

  • | KBC Video
    136 views

    Tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi imewakamata washukiwa saba kati ya 13 kuhusiana na madai ya ufisadi kwenye kashfa ya ununuzi wa bidhaa za shilingi milioni 58.56 katika serikali ya kaunti ya Isiolo. Tume hiyo imedhibitisha kuwa uchunguzi huo unahusiana na zabuni ya kusambaza magari ya kuzima moto ambayo ilitolewa kwa njia isiyofaa kwa kampuni ya Drescoll katika mwaka wa fedha wa 2018/2019. Washukiwa hao kesho watafikishwa kwenye mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi huko Isiolo. Mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim ana maelezo zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive