Tume ya Jinsia na Usawa Imeanzisha Uchunguzi wa hali ya masomo kwa mtoto wa kike katika Maeneo Kame Nchini ikilenga kaunti 17.Afisa Mkuu Mtendaji Wa tume hiyo Dr.Purity Ngina Akizungumza Kaunti ya Tharaka Nithi, Baada ya kukutana na Maafisa wanaosimamia Elimu kaunti hiyo, amesema Uchunguzi huu ni kusaidia tume hiyo kutoa Ushauri kwa idara za Serikali kuhusu Jinsi kuimarisha Masomo na hali ya kijinsia ya Mtoto wa Kike. Tume hiyo inalenga kuangazia Mazingira ya Mtoto kwa kike kwa Jamii na Shuleni anaposoma, Changamoto za Tamanduni, kupata Maji safi, ndoa na mimba za mapema, afya wakati wa hedhi na Mengi yanayoweza kuadhili Masomo.