Skip to main content
Skip to main content

Tunachokijua kuhusu kutoweka kwa Twaha Mwaipaya

  • | BBC Swahili
    63,509 views
    Duration: 2:48
    Mwanaharakati wa Tanzania, Twaha Mwaipaya, anadaiwa kutekwa nchini Kenya, tukio lililozua wasiwasi miongoni mwa wanaharakati na mashirika ya kutetea haki za binadamu Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa Amnesty International Kenya, Mwaipaya alidaiwa kutekwa Jumapili, Oktoba 25, alipokuwa akisafiri kwa teksi katika eneo la Kamulu, karibu na Nairobi. Madai hayo yameibua maswali kuhusu alipo, waliohusika na sababu za kutoweka kwake. Lakini Twaha Mwaipaya ni nani? Na kwa nini tukio hili limezua wasiwasi kuhusu usalama wa wanaharakati katika Afrika Mashariki? Hadi wakati taarifa hii inaandaliwa, BBC Swahili ilikuwa bado haijapata majibu kutoka kwa serikali ya Kenya baada ya kuitafuta ili kupata msimamo wake. Mwandishi wa BBC @mariammjahid na taarifa zaidi - - 🎥 @brianmala #bbcswahili #utekaji #chadema #kenya #tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw