Skip to main content
Skip to main content

Uchunguzi waonyesha waathiriwa wa mauaji Ishiara walipigwa risasi na kuvuja damu nyingi

  • | Citizen TV
    985 views
    Duration: 1:09
    Upasuaji wa maiti umethibitisha kuwa watu wawili waliouawa wakati wa maandamano eneo la ishiara kaunti ya Embu walifariki kwa kuvuja damu kufuatia majeraha ya risasi. Uchunguzi wa maiti uliofanyika hospitali ya rufaa ya kaunti ya embu leo na kuongozwa na mpasuaji wa maiti wa serikali dkt. Grace midigo, ulionyesha kuwa mmoja alipata jeraha la risasi shingoni huku wa pili alisalia na risasi iliyopitia mdomoni. Risasi hiyo ilitolewa na kukabidhiwa maafisa wa upelelezi .