- 2,815 viewsDuration: 2:09Uchunguzi wathibitisha wanaume wawili waliuawa kwa risasi Embu Uchunguzi wa maiti za wanaume wawili waliouawa wakati wa vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa Naibu Rais huko Embu umethibitisha kuwa walifariki kutokana na majeraha ya risasi. Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa maiti, mmoja wa vijana hao alipigwa risasi kichwani huku mwingine akifariki baada ya kupigwa risasi mguuni. Familia za marehemu hao sasa zinataka uchunguzi wa kina kufanywa na maafisa wa polisi wanaodaiwa kuhusika kukamatwa.