- 1,248 viewsDuration: 2:56Idadi kubwa ya watu ilishuhudiwa kwenye uchaguzi wa viongozi wa mashinani wa chama cha UDA katika kaunti 17 zilizoshiriki zoezi hilo. Viongozi mbalimbali wa chama cha UDA wametaja hali hiyo kama ishara kuwa chama hicho kimepata uungwaji mkono hata katika ngome za jadi za vyama vingine kama vile ODM na Wiper. Chama cha UDA kinalenga kuchagua viongozi wa ngazi za chini mashinani. Na kama anavyoarifu Chrispine Otieno, Viongozi walioibuka washindi wanatambuliwa kielektroniki baada ya shughuli hiyo kukamilika saa kumi na moja jioni.