- 310 viewsDuration: 2:58Wakulima wa mahindi katika kaunti ya Trans Nzoia wanakabiliwa na changamoto mpya ambayo huenda ikaongeza gharama ya uzalishaji msimu huu. Hali hii inatokana na wengi wao kulazimika kulima tena mashamba yao baada ya magugu kumea wakisubiri mbolea. Uhaba wa mbolea nchini umewasababisha wakulima kuchelewa kupanda wakihofia kugharamika zaidi ili kukuza chakula msimu huu. Wizara ya kilimo imekiri kuwepo na uhaba huo na kusema kuwa shehena nyingine ya mbolea aimewasili nchini na itaanz akusambaziwa wakulima mara moja.