- 3,664 viewsDuration: 3:05Kwa siku nyingine, jiji la Nairobi limesalia chini ya ulinzi mkali wa polisi huku vizuizi vikiwekwa katika maeneo mbalimbali kuzuia maandamano ya Saba Saba. Vizuizi hivyo katika barabara kadhaa za kuingia na kutoka jijini vilitatiza pakubwa shughuli za usafiri. Vitengo mbalimbali vya maafisa wa usalama vilionekana vikifanya doria katika maeneo mengi ya jiji.