Skip to main content
Skip to main content

Uongozi wa chama cha Ford Kenya wasema chama hicho hakitavunjwa ili kuungana na UDA

  • | Citizen TV
    1,001 views
    Duration: 1:11
    Chama cha FORD Kenya kimekataa wito wa kuvunjwa kwa vyama tanzu ndani ya muungano unaotawala, kikieleza kuwa hatua hiyo itazima demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Katibu Mkuu wa chama hicho, John Chikati, ameshutumu baadhi ya viongozi wa chama cha UDA kwa kutoa vitisho vya mara kwa mara vinavyolenga kuvishinikiza kuvunjwa kwa vyama vidogo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.