Skip to main content
Skip to main content

UREJESHI WA MIKOKO KWA KUTUMIA NJIA ASILI BADALA YA KUPANDA OVYO OVYO

  • | KNA Video
    39 views
    Duration: 2:44
    Katika juhudi za kuimarisha utunzaji wa mikoko katika maeneo loevu, wadau wa mazingira humu nchini sasa wanahimiza umma kukumbatia urejeshi wa mikoko kwa kutumia njia za asili badala ya kupanda mikoko ovyo ovyo. Wakizungumza katika warsha ya uhamasishaji wa wanahabari kuhusu urejeshi wa mikoko iliyoandaliwa na shirika la WWF Kenya mjini Mtwapa, kaunti ya Kilifi wadau hao wamesema kuwa tofauti na miti mingine mikoko sio lazima ipandwe kwani inao uwezo wa kukua yenyewe katika mazingira yanayofaa.