Shule zote za msingi katika kaunti ya Lamu hazina mabasi ya shule. Hali hii imesababisha wanafunzi na walimu, kukodisha mabasi ya shule za upili wakati wanaposafiri kushiriki michezo na hafla nyingine za elimu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa michezo ya riadha kwa wanafunzi wa shule za msingi eneo la Mpeketoni, Spika wa Bunge la Lamu, Azhar Mbarak, amesikitika kuona baadhi ya wanafunzi wakipanda bodaboda kufika kwenye uwanja wa michezo. kulingana naye, Hali hiyo inahatarisha usalama wao, hasa watoto wa kike.