Skip to main content
Skip to main content

Usajili wa bima ya SHA Busia wapuuzwa na jamii

  • | Citizen TV
    196 views
    Duration: 2:13
    Idadi ya wakazi katika kaunti ya Busia wakiwemo wakongwe ambao hawajajiandikisha katika bima ya kitaifa ya SHA bado iko juu, huku wakazi wakihimzwa kuendelea kujiandikisha katika bima hiyo ya kitaifa ili kupunguza gharama ya matibabu. Spika wa bunge la Busia mhandisi Fredrick Odilo amesikitika kuwa wakazi hujiandikisha katika bima hiyo wakati wanapougua, na baada ya kupata matibabu wanakosa kulipia ada ya bima hiyo, swala linalopelekea malimbikizi ya madeni katika bima hiyo ya kitaifa. Akizungumza kwenye hafla ya kufungua rasmi makafani ya kibinafsi viungani mwa mji wa Busia, spika huyo amewahimiza machifu na manaibu wao kutembea maeneo ya vijijini ili kuwahamasisha na kuwahimiza wakazi wakiwemo kujisajili.