Ushuru wa Trump waanza kutekelezwa

  • | BBC Swahili
    1,939 views
    Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Marekani imeanza kupokea mabilioni ya pesa wakati ambapo ada mpya za kutuma bidhaa Marekani zimeanza kutekelezwa. Zaidi ya mataifa 90 kote duniani yataathirika na ushuru huo. Dakika chache kabla ya saa sita usiku, Trump aliandikaa kwenye mtandao wake wa kijamii kwamba mabilioni ya dola yalikuwa yameshaanza kuingia Marekani . Mataifa matano ya Afrika Lesotho , Afrika kusini , Nigeria, zambia na Zimbabwe yameathirika. Afrika kusini sasa itatozwa ushuru wa asilimia 30 kwa bidhaa wanazotuma Marekani. Serikali ya Pretoria inasema itaendelea na biashara na Washington licha ya hali hiyo. Je hii itaaathiri vipi uchumi wa mataifa husika? @RoncliffeOdit anaangazia hili na mengine Mengi leo saa tatu usiku katika Dira ya Dunia TV, itakayokujia mubashara kupitia ukurasa wa YouTube BBC Swahili. #bbcswahili #marekani #ushuru Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw