Afya ya akili inaendelea kuwa changamoto duniani kote, huku ripoti zikionyesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne wanaotafuta huduma za afya huenda anaishi na hali ya afya ya akili.
Run vcrs
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Mafunzo ya Uongozi kuhusu Afya ya Akili unaowaleta pamoja washiriki kutoka nchi 17, Katibu katika wizara ya Afya Mary Muthoni, amesema takwimu hizo zinaashiria kuongezeka kwa mzigo kwa mifumo ya huduma za afya.
Mpango huo wa wiki mbili, unalenga kuimarisha uwezo wa uongozi katika sekta ya afya ya akili katika eneo hili.