Skip to main content
Skip to main content

Utata wa kifo cha mtoto Gilgil wazua kizaazaa hospitalini

  • | Citizen TV
    15,119 views
    Duration: 2:32
    Kizaazaa kilishuhudiwa katika makafani ya hospitali ya Gilgil baada ya familia moja kukabiliana na walimu kuhusiana na kifo cha mwana wao wa miaka mitatu. Mwanafunzi huyo wa chekechea alifariki katika hali tatanishi akiwa shuleni siku ya Ijumaa. Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa maiti, mtoto huyo alikosa pumzi na kufariki baada ya kuzama majini. Familia hiyo inataka uchunguzi wa kina, ikisema walimu wa mwanafunzi huyo waliwapigia simu na kutoa taarifa mbili tofauti kuhusu kifo chake.