Skip to main content
Skip to main content

Utendakazi wa Serikali: Kindiki apigia debe miradi, akutana na wanawake Laikipia

  • | Citizen TV
    368 views
    Duration: 1:08
    Naibu rais Profesa Kithure Kindiki, ameendelea kupigia debe utendakazi wa serikali ya Kenya kwanza,na kusema kamwe hatazembea katika kutekeleza majukumu ya kumsaidia RAIS William Ruto,kukamilisha miradi mbalimbali nchini. Kindiki, ameitetea serikali kuwa imefanikisha ujenzi wa masoko katika kaunti ya Laikipia ili kusaidia Juhudi za wafanyabiashara wanaochangia katika ukuaji wa uchumi. Kindiki ameyasema hayo alipowahutubia akina mama zaidi ya 1,500 kutoka Kaunti ya Laikipia waliokongamana kijijini Irunduni katika kaunti ya Tharaka Nithi.