- 926 viewsDuration: 3:36Hali ya utulivu ilishuhudiwa katika kaunti mbalimbali nchini wakati wa maadhimisho ya Saba Saba. Jijini Mombasa, idadi ndogo ya waandamanaji walifanya maandamano ya amani wakitaka kukomeshwa kwa mauaji ya kiholela na serikali kuheshimu Katiba. Katika Nyeri County na Nakuru County, shughuli za biashara ziliendelea kama kawaida, ingawa huduma za usafiri kati ya Nakuru na Nairobi ziliathirika.