- 374 viewsDuration: 4:01Kuendelea kwa shughuli za kibinadamu karibu na misitu ya kaya katika kaunti za Kwale na Kilifi kumeonekana kusababisha unyakuzi wa ardhi za misitu hiyo. Misitu miingine pia ikiingiliwa na wakulima na wafugaji na kusababisha uharibifu mkubwa wa turathi hizo za kitaifa zinazolindwa kwa sababu za kitamaduni na mazingira. Sasa baadhi ya Wazee wa Kaya hizo wamekata shauri na kuanza kuweka alama za mipaka ili kuzuia uharibifu huo