- 4,949 viewsDuration: 3:39Kwa miaka mingi, uwanja wa Kamukunji ulitambulika kwa mikutano ya kisiasa ambayo mara nyingi ilishuhudia ghasia. Ila ni chimbuko la maandamano na mikutano ya kisiasa iliyochangia kurejea kwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa nchini. Lakini katika muda wa mwaka mmoja uliopita, uwanja huu wa kihistoria umepata sura mpya. Wakazi ambao wakati mmoja walitoroka vitoa machozi sasa wanajiandaa kuwapeleka watoto wao kwa viwanja vya michezo na kituo cha jamii.