- 5,851 viewsDuration: 2:11Wakazi wa Kaunti ya Wajir wameibua wasiwasi kufuatia zoezi linaloendelea la upangaji na upimaji wa ardhi inayohusishwa na mpango wa upanuzi wa uwanja wa ndege, wakidai kuwa hatua hiyo inafanyika bila ushirikishwaji wa umma wala fidia kwa watakaoathirika. Wakaazi pamoja na viongozi wa eneo hilo sasa wanaishutumu serikali kwa kile wanachodai ni unyakuzi wa ardhi ya jamii kwa nguvu, hali inayoweka mamia ya familia katika hatari ya kuhamishwa. Wanatoa wito kwa serikali ya kitaifa kusitisha mara moja zoezi hilo na badala yake kuwashirikisha wakazi walioathiriwa kupitia taratibu za kisheria. Wakiongozwa na Mwakilishi wadi wao Adan Bulle, wakazi hao wanasisitiza kuwa licha ya kuunga mkono miradi ya maendeleo, ni lazima ifuate utaratibu unaotambuliwa kisheria, ikiwemo ushirikishwaji wa umma, fidia ya haki, na mazungumzo ya uwazi.