Skip to main content
Skip to main content

Video feki za AI katika maudhui ya kisiasa

  • | BBC Swahili
    8,438 views
    Duration: 1:48
    Picha na video za wanawake zinazotengenezwa kwa kutumia akili mnemba (AI) zinazidi kuonekana kwenye machapisho ya kisiasa mtandaoni. Mara nyingi, wanawake hao huonyeshwa kwa namna inayosisitiza mvuto wao wa kimapenzi. BBC imechunguza machapisho hayo na kubaini kuwa kuna sababu mbalimbali zinazowafanya watu wayatengeneze. Baadhi hutumia picha hizo kujaribu kuchafua taswira ya vuguvugu fulani la kisiasa, huku wengine wakilenga kupata fedha kwa kutumia umaarufu wa machapisho ya kisiasa. BBC haikuweza kubaini watu walio nyuma ya akaunti hizo. Hata hivyo, Meta na TikTok zilisema zimeondoa maudhui yaliyokiuka kanuni zao. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw