- 611 viewsDuration: 1:55Baadhi ya vijana huko Mombasa wamefanya matembezi ya amani kutoka eneo la Treasure Square hadi afisi za tume ya uchaguzi huko Kizingo eneo bunge la Mvita. Vijana hao chini ya mwavuli wa tuko kadi wamesema wataendelea kutoa hamasisho mjini Mombasa wakilenga kusajili zaidi ya wapigakura 450,000 ifikiapo Agosti. Katika hamasisho hilo baadhi ya wale waliojisajili hii leo kwa mara ya kwanza wamesema kiu ya uongozi bora ndio ilichochea wao kujitokeza kujisajili. Pia wanairai tume ya uchaguzi kufanya hamasisho zaidi ili kuongeza idadi ya wapiga kura wapya.