- 2,472 viewsDuration: 3:30Vijana katika maeneo mbalimbali nchini wanaendelea kujitokeza ili kusajiliwa kama wapigakura kwenye uchaguzi mkuu ujao. Kupitia kampeni ya "Niko Kadi" inayonuia kuwasukuma vijana kujisajili kwa wingi ili kubadilisha uongozi mwaka wa 2027, vijana waliofika katika vituo mbalimbali vya IEBC wameelezea ari yao ya kuwa na usemi kuhusu uongozi wa nchi na kutumia kura yao kama silaha ya kushinikiza uongozi bora.