- 188 viewsDuration: 2:13Katika juhudi za kukabili visa vya ujangili katika bonde la Kerio zinazotokana na wizi wa mifugo, serikali kupitia kituo cha kitaifa cha kukabiliana na ugaidi (NCTC) imeanzisha mpango wa kuwapatia mafunzo vijana walioacha wizi wa mifugo katika eneo hilo. Hatua hiyo inalenga kuwasaidia na kuwageuza kimawazo vijana waliokuwa majangili . Hadi sasa, vijana 16 wamepata mafunzo yanayolenga kuwawezesha kujiinua maishani kwa kufanya kazi zenye manufaa kama kilimo.