- 298 viewsDuration: 1:31Jumla ya timu arubaini za wanaume na wanawake kutoka eneo bunge la Roysambu hapa Nairobi zitapambana kuwania taji la michuano ya daktari Faith Mwaura iliyoanza jana Jumapili uwanjani Kahawa West. Lengo kuu la mchuano huo utakaomalizika Mei 3, ni kukuza vipaji vya vijana mashinani sawa na kuwaepusha na kujiunga na makundi ya uhalifu. Timu zote zinazoshiriki zilituzwa sare na mipira wakati wa uzinduzi ili kupunguza changamoto za uhaba wake.