Viongozi Tana River wahimiza umuhimu wa amani nchini

  • | Citizen TV
    81 views

    Baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya Tana River wamehimiza jamii mbali mbali ZInaoishi kwenye kaunti hiyo kudumisha amani wakati huu na kabla ya uchaguzi mkuu. Viongozi hao ambao walizungumza mjini Madogo katika hafla moja ya harusi walisema kaunti ya Tana River ina historia mbaya ya vita vya kijamii ambavyo vimepelekea kupotea kwa maisha ya watu wengi kutokana na sababu za kisiasa na ugomvi kuhusu umuliki wa ardhi. Aidha waliwatahadharisha wenyeji kujiepusha na viongozi wanaotumia migawanyiko ya jamii kwa manufaa yao ya kisiasa.