- 5,378 viewsDuration: 1:29Viongozi wa kenya kwanza wamemshambulia rais mstaafu uhuru kenyatta, wakisema matamshi yake ya hivi karibuni dhidi ya rais william ruto ni ya kikabila na yanaweza kuwagawa wakenya. Wamemtaka kuheshimu nafasi yake kama rais mstaafu na kuacha kuligawanya taifa. Wakizungumza narok kusini, kwenye mpango wa kuwawezesha vijana, viongozi hao, mbali na kumpigia kampeni rais william ruto, pia wamewataka viongozi wa kidini kote nchini kuhubiri umoja na kuwakanya wanasiasa wanaoendeleza siasa za kikabila. Sawia na kauli zilizotolewa na viongozi wengine wa kenya kwanza katika kaunti za kericho na Kakamega.